Mapambo na marembo katika Ramadhaan

Swali: Leo imekuwa ni jambo la kawaida kati ya baadhi ya? watu kuremba, kupamba na kuyang?arisha manyumba yao kwa ajili ya kuonyesha furaha ya Ramadhaan. Wapo wengine ambao wanazifanya maalum baadhi ya sehemu nyumbani kwa ajili ya mapambo na kupaka rangi na kupanga chakula cha futari na cha daku. Je, inafaa?

Jibu: Hili halina msingi. Hakuna tofauti kati ya Ramadhaan na miezi mingine inapokuja katika kutengeneza mambo ya nyumbani. Ramadhaan haitakiwi kufanywa maalum kwa chochote katika hayo. Ramadhaan haitakiwi kufanywa maalum kwa kuyapamba manyumba, mapazia na maonekano. Ramadhaan inatakiwa kufanywa maalum kwa ajili ya ?ibaadah, tawbah, kuswali Tarawiyh na swalah ya usiku na waislamu wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=DoIP75VDYCo&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 27/05/2017