Maoni yenye nguvu kuhusu kutikisa kidole katika Tashahhud kwa mujibu wa Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Unasemaje juu ya kutendea kazi jambo la kutikisa kidole katika Tashahhud?

Jibu: Maoni yaliyo sahihi zaidi kwangu kuhusiana na suala ka kutikisa kidole ni kwamba mtu anatakiwa kukitikisa kila pale ambapo anaomba du´aa. Kwa mfano pale anaposema:

رب اغفر لي

“Ee Mola! Nisamehe!”

na huku anatikisa.

وارحمني

“Nirehemu.”

na huku anatikisa. Kila sentesi ya du´aa anatakiwa kutikisa kidole. Katika Tashahhud:

السلام عليك أيها النبي

“Amani ya Allaah iwe juu yako, ee Mtume… “

Hii ni du´aa na hivyo anatakiwa pia kutikisa kidole.

السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين

 “Amani ya Allaah iwe juu yetu na juu ya waja wa Allaah walio wema.”

hapa pia anatakiwa kutikisa kidole.

اللهم صل على محمد

“Ee Allaah! Msifu Muhammad… “

anatikisa kidole.

اللهم بارك على محمد

“Ee Allaah! Mbariki Muhammad… “

anatikisa kidole.

أعوذ بالله من عذاب جهنم

“Najilinda kwa Allaah kutokamana na adhabu ya Jahannam… “

anatikisa kidole.

ومن عذاب القبر

“… na kutokamana na adhabu ya kaburi.”

anatikisa kidole. Kilicho muhimu ni kwamba anatikisa kidole chake wakati wa kila du´aa. Kwa ajili hii imepokelewa katika Hadiyth:

“Alikuwa akikitikisa na akiomba du´aa kwacho.”

Maana iko wazi. Kwa sababu anakinyanyua kumwelekea Allaah (´Azza wa Jall) ambaye ndiye anamuomba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1490
  • Imechapishwa: 04/02/2020