Maoni yenye nguvu kuhusu kuoga siku ya ijumaa

Swali 26: Josho la siku ya ijumaa ni wajibu au imependekezwa tu?

Jibu: Maoni sahihi yanayopelekea dalili ni kwamba ni wajibu. Hayo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy katika “as-Swahiyhayn” na wengineo ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Josho la siku ya ijumaa ni wajibu kwa kila mwenye kuota.”

Wale wenye kuona kuwa sio wajibu wanastadili kwa Hadiyth ya al-Hasan bin Samurah:

“Mwenye kutawadha siku ya ijumaa, basi ni sawa, na mwenye kuoga basi kuoga ndio bora.”

Kutokana na ninavojua ni kwamba ni kupitia Hadiyth ya al-Hasan bin Samurah. Kuna tofauti kuhusu kusikia kutoka kwake. Jengine ni kwamba iwapo itakuwa imethibiti hakuna dalili inayosema kuwa kuoga siku ya ijumaa sio lazima. Kwa sababu kutenda jambo ambalo ni bora ndio bora zaidi kuliko kuliacha. Hayo yamesemwa na Muhammad bin Hamz (Rahimahu Allaah) katika “al-Mahallaa”. Isitoshe kuna Hadiyth katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja akitawadha kisha akaenda msikitini, basi anapata kadhaa na kadhaa.”

Hakutaja kuhusu kuoga. Hadiyth hii ina mkato kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah ambayo ndani yake inasema kwamba mja akioga na akaenda ijumaa katika saa ya kwanza, basi anapata ujira fulani na fulani, au atakayeoga akaenda ijumaa, basi husamehewa yaliyo kati ya ijumaa mbili au Hadiyth yenye maana kama hiyo. Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 74
  • Imechapishwa: 25/10/2019