Maoni ya sawa ni kwamba imesuniwa kufunga siku kumi za Dhul-Hijjah

Swali: Je, imethibiti kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga siku kumi za Dhul-Hijjah?

Jibu: Haikuthibiti. Imepokelewa kutoka kwake kwa cheni ya wapokezi ilio na kasoro. ´Aaishah amesema kwamba hakuwa akizifunga na imepokelewa kutoka kwa Hafaswah kwamba alikuwa anayafunga. Lakini katika cheni ya wapokezi wake kuna kasoro. Lakini maoni ya sawa ni kwamba ni Sunnah kuyafunga. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna masiku yoyote matendo mema ndani yake yanapendwa zaidi na Allaah kama  masiku haya kumi.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake. Kadhalika ameipokea kwa cheni ya wapokezi ilio nzuri:

“Hakuna masiku yoyote ambayo ni matukufu zaidi mbele ya Allaah na ambayo yanapendwa zaidi Kwake kama masiku haya kumi. Hivyo kithirisheni ndani yake kusema “Laa ilaaha illa Allaah”, “Alhamdulillaah” na “Allaahu Akbar”.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) anasema kwamba hatambui kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anayafunga. Vilevile imepokelewa kutoka kwa Hafswah kwamba  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiyafunga. Lakini katika cheni ya wapokezi wake kuna baadhi ya dosari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/6684/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%8A%D8%A7%D9%85-%D8%B9%D8%B4%D8%B1-%D8%B0%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D8%AD%D8%AC%D8%A9
  • Imechapishwa: 14/08/2018