Maoni ya maimamu wakaguzi juu ya mwanamke kuyatembelea makaburi

Swali: Je, inafaa kwa wanawake kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Wanazuoni wametofautiana juu ya suala hili. Kikosi cha wanazuoni walio wengi wanaona kuwa inafaa kwa wanawake kuyatembelea makaburi. Wamesema kuwa mwanzoni Hadiyth zilikataza ambapo wakakatazwa wanamme na wanawake. Kisha ikaja ruhusa kwa wote.

Maoni ya pili ya wanazuoni ni kwamba wanawake wamekatazwa na kwamba ilipokuja idhini kwa wanamme yakaja makatazo kwa wanawake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale wenye kuyawekea mataa.”

Maoni ya sawa ni kwamba wamekatazwa. Haya ndio yamehakikiwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na maimamu wa Da´wah (Rahimahumu Allaah).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 20/11/2021