Maoni ya Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kupeana mikono baada ya swalah

Swali: Vipi kuhusu kutoa salamu na kupeana mikono baada ya kumaliza swalah sawa iwe ni swalah ya faradhi au swalah ya Sunnah?

Jibu: Kuhusu kutoa salamu baada ya kumaliza kuswali, salamu ya swalah inatosha. Kwa sababu mtu akitoa salamu kuliani kwake na kushotoni kwake, amekwishatoa salamu na inatosha. Lakini mazowea na maruwa imezoeleka kwamba mtu anapomaliza kuswali na khaswa khaswa swalah ya sunnah, basi anawatolea salamu walioko kuliani kwake na kushotoni kwake. Wanaona hivi ni katika utimilifu wa muruwa, mahaba na mapenzi. Mimi kwa mtazamo wangu naona kuwa hakuna neno kufanya hivo. Kwa sharti mtu asiitakidi kuwa kitendo hicho kimewekwa katika Shari´ah kufanywa baada ya swalah. Bali tu ahisi kuwa anatoa salamu kwa sababu hivi sasa amemaliza kupeana mikono na kujuliana hali. Ama pale mara ya kwanza alikuwa ameshughulishwa na Tahiyyat-ul-Masjid au sunnah ya Raatibah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1071
  • Imechapishwa: 23/03/2019