Maoni sahihi ni kwamba inafaa kwa mwenye hedhi kusoma Qur-aan

Swali: Sisi ni wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha wanawake. Tunayo silebasi ya kuhifadhi juzu ya Qur-aan. Wakati mwingine wakati wa mtihani unakutana na ada ya mwezi. Je, inasihi kwetu kuandika Suurah kwenye karatasi na kuihifadhi?

Jibu: Inafaa kwa mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kusoma Qur-aan kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanazuoni kwa sababu ya kutokuwepo chenye kujulisha juu ya makatazo ya kufanya hivo. Lakini afanye hivo bila kugusa msahafu. Inafaa kwao wawili kuigusa nyuma ya kizuizi kama mfano wa nguo safi na mfano wake. Vivyo hivyo inahusu karatasi aliyoandika Qur-aan ndani yake wakati wa haja ya kufanya hivo.

Kuhusu mwenye janaba haifai kwake kusoma Qur-aan mpaka akoge. Kwa sababu kumepokelewa Hadiyth Swahiyh inayofahamisha juu ya kukataza. Haijuzu kumlinganisha mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi juu ya mwenye janaba. Kwa sababu muda wao unarefuka tofauti na mwenye janaba ambaye kuna wepesi kwake kuoga katika wakati wowote kuanzia pale anapomaliza kutoka katika yale mambo yanayowajibisha janaba.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/208)
  • Imechapishwa: 05/09/2021