Maoni mawili kuhusu Aayah inayozungumzia uso wa Allaah

Swali: Allaah (Ta´ala) amesema:

وكُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa uso Wake.” (28:88)

Nini maana ya Aayah hii?

Jibu: Wafasiri wa Qur-aan wana maoni mawili kuhusu maana ya Aayah hii ambazo amezitaja Imaam at-Twabariy katika “Tafsiyr” yake kwa kusema:

1 – Wametofautiana maana ya:

 إِلَّا وَجْهَهُ

“… isipokuwa uso Wake.”

baadhi yao wamesema kwamba kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa Yeye tu.

2 – Wengine wakasema kuwa maana yake ni kwamba isipokuwa tu kile kilchofanywa kwa kukusudia uso Wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/كُلُّ-شَيْءٍ-هَالِكٌ-إِلَّا-وَجْهَهُ
  • Imechapishwa: 17/06/2022