Maoni mawili juu ya mwanamke mwenye damu ya uzazi

Swali: Nimejua kuwa muda wa damu ya uzazi ni siku arubaini. Lakini wakati mwingine inaweza kwenda mpaka siku sitini na sijui baada ya siku arubaini niswali au nisiswali. Naomba uniwekee wazi ili nisije kuziharibu swalah zangu.

Jibu: Wanachuoni (Rahimahumu Allaha) wametofautiana juu ya wingi wa muda wa damu ya uzazi. Wako waliosema kwamba muda wake mwingi ni siku arubaini. Kujengea juu ya maoni haya damu ikizidi siku arubaini, ikiafikiana na masiku yake ya kupata hedhi kabla hajashika mimba, basi atajizuia [na ´ibaadah]. Vinginevyo itakuwa ni damu fasidi. Katika hali hiyo atatakiwa kuswali, kufunga na atakuwa ni halali kwa mume wake. Haya ndio madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) kwa mujibu wa wafuasi wake.

Maoni ya pili wanaona kuwa wingi wake ni siku sitini na wanaona kwamba midhali muda inatoka katika sura moja na haijabadilika, basi asubiri hadi siku sitini. Haya ni madhehebu ya ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) kwa mujibu wa wafuasi wake. Kujengea juu ya maoni haya zikitimia siku sitini na damu ikawa ni yenye kuendelea kutoka, basi tutasema kwa kile kilichozidi juu ya siku sitini kama tulivyosema kwa kile kilichozidi juu ya siku arubaini. Ikikutana na masiku yake ya kupata ada ya kila mwezi basi hiyo ni hedhi. Isipokutana na masiku yake ya kupata ada basi hiyo ni damu fasidi. Katika hali hiyo atatakiwa kujisafisha, kuswali na kufunga.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (59) http://binothaimeen.net/content/1354
  • Imechapishwa: 22/11/2019