Maombolezo ya kipumbavu ya Raafidhwah ´Aashuuraa´

Miongoni mwa upumbavu wao ni kwamba wanahuzunika na kuomboleza kwa mtu ambaye ameuawa kwa miaka mingi. Ni jambo linalotambulika kwamba kitendo kama hicho ni miongoni mwa mambo aliyoyakataza Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa mtu atafanya hivo baada tu ya kufa kwa mtu. Imesihi kupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba ameseam:

“Si katika sisi yule mwenye kujipiga mashavu na akachanachana nguo zake na akaita wito wa kipindi cha kikafiri.”[1]

Haya ndio yanayofanywa na watu hawa. Wanajipiga kwenye mashavu, wanararua nguo zao, wanaita kwa wito wa kipindi cha kikafiri na mengineyo yaliyokatazwa baada ya mtu kufariki kwa miaka mingi. Kitendo hicho lau kingefanywa punde tu baada ya kufa kwake basi ilikuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa yaliyoharamisha. Mtu asemeje kuona kinafanywa baada ya miaka mingi baadaye?

Inatambulika kwamba wako Mitume na wengine ambao ni bora kuliko al-Husayn ambao waliuawa kwa dhuluma kabisa. Baba yake aliuawa kwa dhuluma na yeye ni bora kuliko yeye. ´Uthmaan bin ´Affaan aliuawa na kuuliwa kwake ndio ilikuwa mwanzo wa fitina kubwa iliojitokeza baada tu ya kufa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Shari na ufisadi uliopelekea kuuawa kwake ni mkubwa kuliko matokeo yaliyopelekea kuuawa kwa al-Husayn. Wengine pia waliuawa na wakafa na hakuna yeyote ambaye alifanya matanga wala kuomboleza baada ya kupita muda mrefu baada yake. Hakuna wengine wanaofanya hivi isipokuwa tu hawa wapumbavu ambao lau wangelikuwa ndege basi wangelikuwa tai na kama wangelikuwa wanyama wafugwao basi wangelikuwa punda.

Mfano mwingine ni kwamba baadhi yao wanakataa kutumia kuni za mti wa Tamarisk[2]. Wanadai kwamba wamefikiwa na khabari kwamba damu ya al-Husayn ilianguka kwenye mji huo. Ni jambo linalotambulika kwamba haikuchukizwa kutumia kuni za mti huo pasi na kujali ni damu ya mtu gani iliangukia hapo. Mtu asemeje kuhusu miti mingine ambayo haikupatwa na damu?

[1] al-Bukhaariy (2/81).

[2] https://www.nature-and-garden.com/gardening/tamarisk-shrub-flower.html

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/52-55)
  • Imechapishwa: 18/02/2019