Swali: Inafaa kutumia manukato kwa sababu majini hayakaribii sehemu hiyo?

Jibu: Ni nani aliyesema kuwa majini hayakaribii manukato? Nani kasema hivi? Majini wako ardhini na sehemu mbalimbali kukiwemo sehemu za manukato. Kitu kinachoyafukuza majini ni kumdhukuru Allaah. Unapotaka kuyafukuza majini basi mdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na sio manukato.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17346
  • Imechapishwa: 13/12/2017