Manong´oneza ya nafsi ambayo mtu ataadhibiwa kwayo


Swali: Ni yepi yale maongezi ya ndani ya nafsi ambayo mtu anaadhibiwa kwayo na ambayo mtu haadhibiwi kwayo?

Jibu: Maongezi ya ndani ya nafsi ambayo mtu anaadhibiwa kwayo ni yale ambayo mtu ameegemea kwayo, akayaamini na akayaazimia. Haya ataadhibiwa kwayo. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha yule ambaye atapata ndani ya nafsi yake kitu katika wasiwasi, basi amtake kinga Allaah na akomeke nayo. Kwa msemo mwingine asitishe kuyafikiria. Ama mtu akiegemea juu ya jambo na akaliamini, huyu anapata dhambi kwa kiasi na vile alivyoinong´oneza nafsi yake. Mtu anajua tofauti na kitu kinachomtokea ghafla na akakiacha na kitu ambacho kimekita imara kwenye akili yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/834
  • Imechapishwa: 25/03/2018