Swali: Kuna mwanamme punde kidogo kabla ya kukojoa anatokwa na manii kutokana nguvu na wingi wa manii yake, hivo ndivo walivosema madaktari. Je, aoge kila…

Jibu: Hapana. Hapo ni pale ambapo yatamtoka kwa matamanio. Lakini manii ya kawaida yanayomtoka pamoja na mkojo au baada ya kukojoa haidhuru. Huu ni ugonjwa.

Swali: Hata kama rangi yake ni ya manii?

Jibu: Ni lazima yamtoke kwa matamanio:

”Manii yako yakitoka kwa matamanio basi oga.”

Ni lazima yamtoke kwa matamanio; ima kwa kujamii, kupapasapapasa, kubusu au kufikiria.

Swali: Kwa hivyo aache kuoga?

Jibu: Hapana. Halazimiki kuoga. Hakuna kinachomlazimu isipokuwa kutamba kwa maji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21639/حكم-خروج-المني-بغير-شهوة
  • Imechapishwa: 03/09/2022