Swali: Nimesikia mlinganizi mmoja akisema ya kwamba Ahl-us-Sunnah, Shiy´ah, Ismaa´iyliyyah na Ibaadhiyyah wote hawa wanaamini kuwa Allaah ndiye Mola wao, Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mtume wao na Uislamu ndio dini yao…[1]

Jibu: Sio sahihi. Huu ni mseto. Huku ni kuchanganya kati ya wapotevu na wale wenye kufuata haki. Hili sio sahihi. Haya ni maneno batili.

Swali: Watu wengi wamedanganyika na maneno yake. Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Hakuna bahati juu ya hilo – Allaah akitaka. Maneno ya Ahl-us-Sunnah yako wazi.

[1] Swaalih al-Mughaamisiy amesema:

“Mimi nitasema kitu ambacho huenda wasithubutu kukisema baadhi ya wanachuoni. Mimi nasema kwa uwazi ya kwamba Ahl-us-Sunnah, Shiy´ah, Ismaa´iyliyyah na Ibaadhiyyah wote hawa wanaamini kuwa Allaah ndiye Mola wao, Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mtume wao na Uislamu ndio dini yao. Wanaposwali, wanaswali kuielekea Ka´bah. Wanaamini kuwa Ka´bah ndio Qiblah chao, Qur-aan ndio kitabu chao, Qiyaamah ndio sehemu walioahidiwa kukusanywa, Pepo ndio thawabu kwa wale watiifu na Moto ndio thawabu kwa makafiri. Isitoshe wanachinja!” http://okaz.com.sa/article/1551430?utm_source=widget&utm_campaign=plottr&utm_medium=related&plottr_widget=ELATEDAR#sthash.cEXXNhqA.dpuf

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://mobile.twitter.com/KSA_Ahmad__/status/880724364362211329/video/1
  • Imechapishwa: 02/07/2017