Mamkuzi ya kuinama hayajuzu

Swali: Sisi Afrika tuko na ada ya kuinama wakati wa kuwasalimia waheshimiwa. Je, inafaa kufanya hivo?

Jibu: Haijuzu kufanya hivo. Kuinama ni kufanya Rukuu´. Haijuzu kufanya Rukuu´ wala Sujuud kumfanyia mwengine asiyekuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Yule atakayewataka muwainamie, basi wakatalieni na wabainishieni kwamba kitendo hicho hakijuzu katika dini yetu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqa%20Afrika-6-12-1440.mp3
  • Imechapishwa: 04/05/2020