Mambo yote uliyotaja kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh ni Bid´ah

Swali 199: Nimesoma fatwa kadhaa ambazo wanafunzi wanakokoteza kutoka pamoja na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Tunamshukuru Allaah kuona kwamba tulitoka pamoja na Jamaa´at-ut-Tabliygh na tukafaidika sana. Lakini tumeona baadhi ya matendo ambayo hayakuthibiti katika Qur-aan wala Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mfano:

1- Watu wawiliwili au zaidi wanaketi msikitini wakikumbushana Suurah kumi za mwisho za Qur-aan na kuyadhibiti matendo haya kwa sura kama hii kila wakati mtu tunapotoka nao.

2- Kufanya I´tikaaf siku ya alkhamisi kwa sifa endelevu.

3- Kuweka kikomo cha masiku ya kutoka ambayo ni siku tatu kwa mwezi, masiku arubaini kila mwaka na miezi mine katika umri wa mtu.

4- Ulinganizi wa pamoja kwa kuendelea baada ya kila bayana.

Ee Shaykh muheshimiwa! Vipi nikitoka pamoja na kundi hili nifanye pamoja nao matendo haya ambayo hayakuthibiti katika Qur-aan wala Sunnah pamoja na kuzingatia kwamba ni vigumu kugeuza mfumo huu? Huu ndio mfumo wao. Tunaomba utuwekee wazi.

Jibu: Matendo uliyoyataja ya kundi hili yote ni Bid´ah. Haijuzu kushirikiana nao mpaka walazimiane na mfumo wa Qur-aan na Sunnah na waachane na Bid´ah.

Ibn Baaz

´Abdul-Aziyz Aalush-shaykh

Fawzaan

Abu Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 413
  • Imechapishwa: 13/01/2020