Swali: Nilimtaliki mke wangu nami wakati huyo nilikuwa na maradhi ya sukari na mengine na nilikuwa katika hali ya khasira nyingi. Na sijui ni mara ngapi nimemtaliki mke huyu kama ni mara moja au zaidi. Mke wangu anasema kuwa nimemtaliki mara tatu na mimi sujui ni mara ngapi. Isipokuwa ninachojua ni kuwa nilitamka Talaka. Anauliza sasa, anataka kumrejea mke huyu. Je, atakuwa ni Halali kwake kwa sasa? Pamoja na kujua kuwa, nimerudi nyumbani sikumkuta. Na mimi nilimkataza asitoke lakini hakujali na akatoka nyumbani. Naomba hukumu ya hilo na naomba nasaha kwa yaliyo na kheri na mimi na uninasihi vipi ntaamiliana na mke wangu?

Jibu: Swali hili lipelekwe mahakamani. Ikiwa mko nje ya Riyaadh, nendeni katika mahakama ya Kishari´ah na apewe swali mmoja katika ma-Qaadhiy. Awepo mke na muulizwe nyote. Na Qaadhiy atafutu kwa kiasi atakavyoona. Ama ikiwa mko ndani ya Riyaadh, njooni katika Daar al-Iftaah wewe na mke wako. Njooni nyote ili mhojiwe na yasajiliwe mtakayoyasema nyote mkiwepo hapo. Lazima yadhibitiwe mambo na si mambo ya juu juu tu kwa njia ya simu. Mambo hayawi namna hii. Lazima yadhibitiwe mambo na yasijiliwe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: www.alfawzan.af.org.sa/node/10060
  • Imechapishwa: 28/02/2018