Swali: Mimi ni mwalimu katika mada ya historia. Wakati fulani inatokea kuwazungumzia vibaya baadhi ya watu. Je, kitendo changu hichi kinazingatiwa ni usengenyi?

Jibu: Wanahistoria daima walikuwa ni wenye kuwataja watu kwa kuandika kama ni wazuri na waovu. Midhali malengo ni kubainisha hali ya mtu huyu basi hakuna neno kufanya hivo. Hata hivyo kuna nukta muhimu. Haijuzu kuzungumzia vile vita na mivutano iliotokea kati ya Maswahabah. Kwa sababu miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kunyamazia yale yaliyotokea kati ya Maswahabah. Mfano wa hayo ni yale yaliyotokea kati ya ´Aliy bin Abiy Twaalib na Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Haijuzu kuingilia kati. Mambo ni kama alivosema ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz:

”Allaah amezisalimisha panga zetu damu zao. Kwa hiyo ni lazima kwetu kuzisalimisha ndimi zetu kwao.”

Ikiwa mtu anasoma historia anaweza kubainikiwa kuwa ´Aliy biy Abiy Twaalib alikuwa karibu zaidi na usawa kuliko Mu´aawiyah, basi anapaswa kutambua kwamba kila mmoja katika wao alikuwa ni Mujtahid. Mujtahid anaweza kupatia na kukosea. Mujtahid kutoka katika Ummah huu akifanya kila anachokiweza kuifikia haki lakini hata hivyo asiifikie, basi anapata ujira kamilifu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakimu akihukumu ambapo akajitahidi akapatia, basi anapata ujira mara mbili. Na akihukumu ambapo akajitahidi akakosea, basi anapata ujira mara moja.”

Mfano wa mambo haya, kama mambo ya vita yaliyotokea kwa Maswabaha, haitakiwi kuyaeneza kabisa kati ya wanafunzi. Kwa sababu yanaweza kujaalia moyoni mwa mtu chuki juu ya baadhi ya Maswahabah. Ni jambo la khatari sana. Tunawapenda Maswahabah wote. Hata hivyo tunaona kuwa baadhi yao ni wabora zaidi kuliko wengine na baadhi yao walikuwa wenye kupatia zaidi kuliko wengine. Lakini hata hivyo tunawapenda wote. Hatumzungumzii yeyote vibaya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49 A)
  • Imechapishwa: 15/01/2021