Mambo mawili ya wajibu, fidia mbili

Swali: Mtu akiacha kitendo cha wajibu cha hajj ni lazima achinje kondoo wawili?

Jibu: Ndio. Kila kimoja ni chenye kujitegemea. Kwa mfano mtu ameacha kurusha vijiwe mpaka ukaisha wakati wake na akaacha kulala Minaa katika masiku ya Tashriyq, kila kitendo cha wajibu kina fidia yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 19/03/2020