Mambo huenda chapchap kwa Jamaa´at-ut-Tabliygh

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Mayahudi wamegawanyika makundi sabini na moja. Manaswara wamegawanyika makundi sabini na mbili. Na Dini hii itakuja kugawanyika makundi sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu.” Wakasema: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni Jamaa´ah.”

Imepokelewa hivo katika Hadiyth ya Mu´aawiyah. Ama kuhusiana na Hadiyth:

Ni lile litakalofuata yale ambayo mimi na Maswahabah wangu waliyomo hivi leo.”

ni dhaifu kwa sababu imepokelewa kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Ziyaad bin An´am. al-Haakim, ambaye anajulikana kuwa mlaini, amesema:

Si hoja yoyote.”

Ni lazima kwa Waislamu kuwa mkusanyiko mmoja. Ni nani aliyetupa idhini ya kuwa makundi mengi? al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kundi limoja, Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kundi limoja. Jamaa´at-ut-Tabliygh imekusanya kati ya Taswawwuf, Bid´ah na ujinga. Mtu akijiunga na wao baada ya ´Aswr wanamlazimisha kutoa darsa Maghrib. Masikini mtu hajui lolote juu ya Dini. Kwa ajili hiyo masikini huyu anaanza kuchanganya mambo

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 09/04/2015