Mambo haya ni katika kumwamini Allaah

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالْآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ

“Ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah.” (02:04)

Katika kuamini Aakhirah kunaingia yale yote aliyoelezea Allaah katika ghaibu zilizotangulia, ghaibu zinazokuja huko mbele, hali za Aakhirah, uhakika na namna ya sifa za Allaah na yale waliyoelezea Mitume katika hayo. Wanaamini sifa za Allaah na uwepo wake na wanaziyakinisha ijapo hawajui namna zilivyo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, sid. 30
  • Imechapishwa: 04/05/2020