Mamangu haswali Fajr kwa sababu ya kutangulia kwangu kwenda msikitini

Swali: Mama yangu anapitwa na swalah ya Fajr na mimi natoka kabla ya adhaana na hivyo siwezi kumuamsha aswali si yeye wala ndugu zangu hawaswali. Je, inajuzu kwangu kummwagia maji au kumfunua shuka anayojifunika? Je, kitendo hichi kinapingana na kumtendea wema mzazi?

Jibu: Namnasihi muulizaji huyu asitoke kwenda msikitini kabla ya adhaana. Midhali wale walioko msikitini ni wenye kumuhitajia, basi asitoke. Abaki nyumbani mpaka waadhini  kwanza, kisha ndio awaamshe. Anatakiwa kutumia njia zote zitazowafanya kuamka. Lakini afanye hivo bila ya usumbufu. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba akimmwagia maji mama yake usoni mwake atamkera. Lakini haidhuru akimfunua shuka kwa upole na utaratifu. Muhimu ni kwamba namshauri asitangulie kwenda msikitini. Bali asubiri mpaka kuadhiniwe na amwamshe mama yake na ndugu zake. Yuko katika kheri.

Swali: Mtu huyu ndiye muadhini wa msikiti.

Jibu: Hakuna tatizo. Aende aadhini kisha arudi na awaamshe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1469
  • Imechapishwa: 16/01/2020