Swali: Mama yangu ananiamrisha kuvua Hijaab. Kwa sababu ya kukataa kwangu hanisemeshi kwa masiku mengi na wala hataki nimzungumzishe. Nichukue msimamo gani juu yake?

Jibu: Mkinaishe kwamba Hijaab ni jambo la wajibu. Asipokinaika basi usimjali juu ya sharti yake. Usimtii katika jambo hilo:

“Si vyenginevyo isipokuwa utiifu unakuwa katika mema. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18073
  • Imechapishwa: 05/08/2019