Mama na wasichana zake kwenda sokoni na dereva wa kiume

Swali: Mimi ni baba na nina watoo ambapo tunakuwa tumeshughulishwa na kazi zetu. Kwa ajili hiyo tunamruhusu dereva aende sokoni, mihadhara ya kidini na ya kiutamaduni pamoja na mke na wasichana wangu. Naomba jawabu la kutosha juu ya kitendo hichi juu ya uhalali au uharamu wake.

Jibu: Ni sawa endapo dereva atakuwa ni mwaminifu na akapanda pamoja nae wanawake wasiopungua chini ya wawili kwenda sokoni. Kilichokatazwa ni kuwa faragha au kusafiri. Haifai kwa dereva kuwa faragha na mwanamke mmoja hata kama itakuwa ni kwenda sokoni. Haifai kwa dereva kusafiri, hata kama watakuwa wanawake wengi, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume asikae faragha na mwanamke isipokuwa awe pamoja naye Mahram na wala mwanamke asisafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Ikiwa kwenda na kurudi ni ndani ya mji huohuo na hatokuwepo kukaa faragha, bali dereva atakuwa na wanawake wasiopungua wawili ilihali dereva huyo ni mwaminifu, hakuna neno juu ya hilo.

Kuhusu dereva asipokuwa mwaminifu kunakhofiwa juu ya shari yake hata kama mwanamke atakuwa pamoja na wanawake wengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (01)
  • Imechapishwa: 09/09/2020