Mwana kumpa pesa mama tajiri


Swali: Ni ipi hukumu kwa mama ambaye sio fakiri anamuomba pesa mwanae. Je, ni wajibu kwa mtoto wake kumpa?

Jibu: Ndio, ampe mama yake na amridhishe. Isipokuwa tu ikiwa kama amemuomba pesa nyingi zenye kumdhuru, katika hali hii sio lazima. Ama kiwango kidogo na kiwango ambacho kinamridhisha mama yake ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13389
  • Imechapishwa: 25/04/2018