Swali: Mara nyingi hutokea katika masomo ya wasichana mama ndiye anawapigia simu masomo na kuongea na mwalimu au mudiri wa masomo kuhusu maendeleo ya msichana wake hapo masomoni. Je, inafaa kwake kufanya hivo au majukumu haya ya kufuatilia maendeleo ya wasichana yanamuwajibikia baba? Ni zipi nasaha zako?

Jibu: Hapana shaka kwamba baba ndiye mwenye majukumu, kama tulivyosoma punde kidogo. Yeye ndiye mwenye majukumu juu ya watoto wake wa kiume na wa kike. Haitakikani kwa mwanamke kujadiliana na mudiri au waprofesa wa masomo. Hili linakuwa kwa baba. Mwanaume anawasiliana na wanaume wenzake na mwanamke anawasiliana na wanawake wenzake. Ama ikiwa anataka kujadiliana na mudiri wa kike wa masomo na waalimu wa kike, ni sawa. Kwani ambaye atasimamia hilo ni mama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1320
  • Imechapishwa: 29/10/2019