Mama anawazuia watoto wasende msikitini na baba yao


Swali: Mwanamke huyu anaishi katika mji na amejaaliwa kupata watoto ambao umri wao ni miaka ni 12, 9 na 7. Baba yao ni mwenye kuhifadhi swalah msikitini na anataka kuwachukua watoto pamoja naye. Lakini hata hivyo nakataa nachelea juu yao kijicho na badala yake wanaswali nyumbani.

Jibu: Wasiwasi huu ni kutoka kwa shaytwaan. Waache waende na baba yao msikitini ili waweze kujifunza swalah pamoja na waislamu. Usiwe na wasiwasi ukachelea juu yao kupatwa na kijicho na mfano wa hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´alaa al-Hawaa´ http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/1436-03-02.mp3
  • Imechapishwa: 03/12/2017