Swali: Mama yangu ananitaka nimpeleke katika nyumba ya kufanya shoo. Nachelea kuwa kuna maovu. Ikiwa atasalimika kutokamana na matari basi hatosalimika kutokamana na mavazi mabaya na uchi. Je, hapo itafaa kwangu kumkatalia kumpeleka mama yangu?

Jibu: Ni wajibu kwako kumkatalia mama yako. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[1]

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖوَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Saidiane katika wema na kumcha Allaah na wala msisaidiane katika dhambi na uadui.” (05:02)

Usimpeleke sehemu ambapo una dhana yenye nguvu kuwa kuna maasi. Hata hivyo mkinaishe. Akikinaika ni vizuri na asipokinaika basi mwambie kuwa si wewe wala yeye haifai kwenda huko na kwamba hufikirii kumsaidia katika madhambi.

[1] al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3