Swali: Mimi ni kijana ambaye nataka kuhiji. Ila mmaa yangu anakataa hilo kwa hoja kwamba anakhofu juu yangu.

Jibu: Ukiwa ni muweza kwa mali yako basi hiji ijapokuwa atakukataza. Isipokuwa ikiwa kama unajua kuwa iwapo utaenda basi mama yako hatoweza kulala usiku wala hatotamani kuishi, katika hali hii tulizana na wala usihiji. Nuia kuwa umekaa kwa ajili yake na kwamba mwaka ujao utahiji. Lakini ikiwa  anakwambia tu usende na unajua kuwa iwapo utaazimia na kuhiji basi hatojali sana, basi fanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/977
  • Imechapishwa: 20/12/2018