Mama anachelewesha hajj kwa sababu ya kuchunga watoto

Swali: Nataka kutekeleza faradhi ya hajj mwaka huu kwa mara ya kwanza. Nimeolewa na nina watoto wadogo. Mdogo wao ana miezi mitano. Naomnyonyesha unyonyeshaji wa kawaida. Lakini hata hivyo ana uwezo wa kuchukua chakula kingine chepesi kandoni na maziwa. Mume wangu amenikatalia kuhiji kwa hoja unyonyaji wa kawaida. Mimi sitaki kwenda nae kwa kukhofia asije kupatwa na ugonjwa na kubadilika kwa hali ya hewa. Sababu nyingine ni kushindwa kujichukulia fungu kubwa la matendo mema kwa sababu atanishughulisha. Pamoja na kuzingatia kwamba kukubali au kutokubali kwa mume wangu kunategemea na fatwa yako. Je, haya ni katika mambo yanayoniruhusu kuacha kuhiji mwaka huu?

Jibu: Mwanamke mwenye hali kama hii inafaa kwake kuchelewa hajj mpaka mwaka ujao kwa sababu zifuatazo:

Ya kwanza: Wanachuoni wengi wanaona kuwa hajj haiwajibiki punde tu mtu anapokuwa na uwezo na kwamba inafaa kwa mtu kuchelewesha pamoja na kuwa na uwezo.

Ya pili: Huyu ni mwenye kuhitajia kubaki ili aweze kuwachunga watoto wake. Kuwachunga watoto wake ni miongoni mwa kheri kubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke ni mchungi katika nyumba ya mume wake na ataulizwa kwa kile alichokichunga.”

Kwa hivyo asubiri mpaka mwaka ujao. Namuomba Allaah amsahilishie jambo lake na amkadirie yaliyo na kheri na yeye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1425
  • Imechapishwa: 25/12/2019