Mali ya ribaa inafanywa nini baada ya mtu kutubia?

Swali: Mtu ambaye alikuwa anataamiliana mu´alama wa Ribaa kisha akatubu kwa hilo, afanye nini na mali hii ya Ribaa?

Jibu: Akikusanyikiwa na mali ya Ribaa na kutubu kwa Allaah na akaacha mu´alama huu, ajikwamue na mali hii kwa kuiweka katika mambo ya kijamii, ni kama mali ambayo imekosa mmiliki. Mali ambayo imepotea na hakuna mwenye umiliki nayo, inatolewa katika mambo ya kijamii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (33) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-10-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014