Mali iliyokusudiwa kununua gari, nyumba na mfano wa hayo ina zakaah?

Swali: Nina mali Benki ambayo imeshafanya zaidi ya mwaka. Makusudio yangu kwa mali hii nataka kununua gari au nyumba ya kueshi ndani yake na makusudio yangu sio biashara. Je, ni wajibu kwangu kutoa Zakaah?

Jibu: Bila ya shaka ina Zakaah. Ikifikisha Niswaab na kufikiwa na Hawl ni wajibu kuitolea Zakaah, kwa makusudio yoyote umeyokusudia, sawa ikiwa ni kwa ajili ya kuoa, kununua gari, kujenga nyumba n.k. Mali iliyoeneza Niswaab na kufikiwa na Hawl ni wajibu kuitolea Zakaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014