Malengo yao ni kuharibu tu


Baadhi ya ndugu wanapokuwa na chuki na bughudha kwa baadhi ya wanafunzi na wanachuoni. Basi utawaona wanakuuliza swali ambapo unalijibu ambapo baadaye wanampachika nalo mtu yule na kwamba wewe unamkusudia yeye. Wanasema kwamba fulani amesema kuhusu fulani kadhaa na kadhaa. Ilihali uhalisia wa mambo ni kwamba wewe hukumkusudia mtu maalum, wewe umejibu tu swali. Wanaongeza chumvi kwamba umemlenga fulani au kundi fulani. Wanahariri kanda na kutunga vitabu na kusema kwamba fulani amesema kuhusu fulani kadhaa na kadhaa. Malengo yao kufanya hivo ni kuharibu baina ya watu na kuleta mpasuko na chuki kati ya wanafunzi. Mimi nakutahadharisheni. Msidanganyike na jambo hili. Tahadharini sana na jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://youtu.be/T8iijs6V0qQ
  • Imechapishwa: 06/10/2018