Malengo ya simu si haya!


Swali: Mimi nimepewa mtihani wa kutazama picha za haramu za wanawake kwenye simu na kwenginepo. Ni ipi njia ya Kishari´ah ya kujinasua na jambo hili?

Jibu: Aache simu. Asitazame kitu. Simu imewekwa kwa ajili ya mazungumzo peke yake. Haikufanywa kwa sababu ya malengo mabaya. Imefanywa kwa sababu ya mazungumzo tu.

Leo simu imekuwa ni njia ya shari isipokuwa wachache waliorehemewa na Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (72) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighassat%20-11-01-1439h.mp3
  • Imechapishwa: 16/12/2017