Malengo Mawili Ya Kuyatembelea Makaburi

Swali: Allaah alimruhusu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutembelea kaburi la mama yake. Je, ni dalili inayofahamisha kutembelea makaburi ya makafiri? Ikiwa mambo ni hivyo kuna du´aa ya mtu kusoma wakati wa kuingia?

Jibu: Kuna malengo mawili ya kuyatembelea makaburi:

1- Mazingatio. Katika hali hii inajuzu kutembelea makaburi ya makafiri. Lengo ni kupata mazingatio na kuyakumbuka mauti.

2- Kuwaombea du´aa. Hili ni jambo maalum kwa waumini. Awaombee du´aa waumini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017