Malaika wanaweza kuwasaidia waislamu katika Jihaad?


Swali: Je, kuteremka Malaika na kupigana pamoja na waumini kumekatika kwa kufa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kuteremka kwao kunawezekana katika Mustaqbal?

Jibu: Inawezekana. Waumini wakiwa na ukweli pamoja na Allaah, Malaika wanaweza kuteremka na kuwasaidia. Haina maana kwamba na wao watashika silaha na kupigana, hapana. Wanathibitisha nyoyo za waumini na kuwapa nguvu na wakati huo huo wanatia khofu katika nyoyo za makafiri:

إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ آمَنُوا ۚ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ

“(Kumbuka) Pale Mola wako Alipowapelekea Wahy Malaika (kuwaambia): “Hakika Mimi Niko pamoja nanyi; basi wathibitisheni wale walioamini. Nitavurumisha kizaazaa katika nyoyo za waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo (zao), na wapigeni (kwa kukata) kila ncha za vidole (vyao).” (08:12)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (71) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13910
  • Imechapishwa: 16/11/2014