Malaika wameumbwa kutokana na nuru na Ibliys kutokana na moto

Swali: Allaah alimuumba Aadam kutokana na udongo, kabla yake akawaumba Malaika na Ibliys alikuwa miongoni mwa Malaika ambaye alimuumba kutokana moto. Ni kwa nini alimuumba kutokana na moto? Allaah amewaumba Malaika kutokana na kitu gani?

Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kwamba amesema:

”Malaika wameumbwa kutokana na nuru, majini wameumbwa kutokana na mwaka wa moto na Aadam amewaumba kutokana na kile kile mlichosifiwa (yaani kutokana na udongo).”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Kuhusu hekima kutokana na jambo hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mwenye kuijua zaidi. Yeye ni Mwingi wa hekima, mjuzi wa kila anachokiumba na kukiweka katika Shari´ah. Hakuna mwenye kupingana na hukumu Yake wala mwenye kurudisha nyuma mipango Yake. Yeye juu ya kila jambo ni muweza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/154)
  • Imechapishwa: 15/03/2020