Swali: Maneno Yake (Ta´ala):

أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ

“Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah… “ (at-Tawbah 09:65-66)

makusudio ni Aayah za Qur-aan au Aayah Zake zote kukiwemo za kilimwengu? Kipi kinachokusudiwa hapa?

Jibu: Aayah za kilimwengu zipo na hazifanyiwi mzaha. Kwa sababi ni zenye kuonekana. Mtu anaona mlima, miti na mito. Hizi hazifanyiwi mzaha. Ni ulimwengu wenye kuonekana. Makusudio ni zile Aayah zenye kusomwa na Wahy wenye kuteremshwa. Ni Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 141
  • Imechapishwa: 23/12/2018