Hebu twende katika hukumu ya kuonekana kwa Allaah hapa duniani. Je, Allaah anaweza kuonekana hapa duniani au hilo ni jambo lisilowezekana? Je, limetokea au halikutokea?

Mapote yote yamekubaliana kuwa Allaah anaonekana usingizini kama alivyonukuu hayo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah isipokuwa Jahmiyyah ndio wamepinga hilo. Hili ni kutokana ususuwavu wao juu ya kuonekana kwa Allaah. Lakini kuonekana kwa Allaah usingizi ni jambo lenye kujuzu kwa mujibu wa mapote mengine yote. Hilo halilazimishi mtu akaona kwa sifa Alizonazo. Mtu kumuona Allaah usingizini kunatokamana na ilivo imani yake. Ikiwa ana I´tiqaad sahihi basi atamuona Mola Wake katika sura nzuri. Na ikiwa I´tiqaad yake ina kasoro basi atamuona Mola Wake kwa sura inayoendana na imani yake. Vivyo ndivyo alivosema Abul-´Abbaas Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/245-246)
  • Imechapishwa: 27/05/2020