Swali: Je, makundi yote yaliyopo hii leo wanaingia katika mapote 72 yaliyoangamia? Je, al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh pia ni katika wao?

Jibu: Kila ambaye ´Aqiydah, mfumo wake na Da´wah yake inaenda kinyume na yale aliyokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake ni katika mapote potevu.

al-Ikhwaan al-Muslimuun wamekusanya mapote yote. Wamewafungulia mlango Raafidhwah, Khawaarij, Zaydiyyah, Mu´tazilah bali mpaka manaswara. Wamekusanya vipote potevu. Hatusemi kuwa ni pote moja – bali wamekusanya mapote!

Jamaa´at-ut-Tabliygh wako karibu na wao. Wametoa kiapo cha utiifu kwa mujibu wa nidhamu za Suufiyyah. Wamefungulia mlango kila kitu na watu wote.

Hapana shaka ya kwamba ni katika mapote potevu. Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) alipoulizwa swali hili alisema:

“Ni katika wao. Kila mwenye kwenda kinyume na ´Aqiydah Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni katika mapote 72. Maana ya “Ummah wangu” ni wale waliomuitikia Allaah na Mtume wake. Ni mapote 73. Kundi lililookoka ni lile lenye kumfuata na wako juu ya ile dini aliyokuwemo. Katika mapote hayo 72 kuna makafiri, wazushi na watenda madhambi.”

Hii ndio mizani. Hii ndio mizani ya kuwapima al-Ikhwaan al-Muslimuun na wengineo. Je, ´Aqiydah, mfumo, Da´wah yao na kupenda na kuchukia kwao kunaafikiana na yale aliyokuwemo Mtume na Maswahabah wake au wana mifumo mingine? Jibu ni kuwa wana mifumo mingine inayopingana kabisa na yale aliyokuwemo Mtume na Maswahabah wake katika ´Aqiydah, mfumo wake na kupenda na kuchukia kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 19
  • Imechapishwa: 05/11/2016