Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) anaonelea kuwa Moto na Pepo vitaisha [kutoweka]. Je, nukuu hizi ni sahihi au ni kumsemea uongo?

Jibu: Enyi ndugu zangu, msitafute maneno yasokuwa na nguvu na mkajishughulisha nayo. Achaneni nayo. Msiyatafute na mkayaeneza. Allaah Hakuwakalifisha nalo. Binaadamu ni mtu. Hupatia wakati fulani na wakati mwingine hukosea. Msitafute makosa na mkajishughulisha nayo.

Baadhi ya watu wanafanya hivi kwa malengo ya kutaka kumtukana Ibn-ul-Qayyim na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Malengo yao ni kutaka kuwatukana kwa makosa haya madogo. Hawaangalii matendo yao makubwa na elimu yao iliyobobea na waliyoyafanya katika kuwanufaisha watu. Haya hawayatazami! Wanatazama vijimakosa vidogo na kuyaanika hadharani kwa kuwa ni maadui wa watu wa kheri. Hawa ni maadui wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na maadui wa Ibn-ul-Qayyim. Pamoja na kwamba upande wa Ibn-ul-Qayyim haikuthibiti kwake kuwa amesema hivi. Aliyazungumzia kama maelezo na si kuwa yeye binafsi anaonelea hivo. Allaah ndiye Anajua zaidi.

Kwa kifupi ni kwamba msitafute maneno yasiyokuwa na nguvu na mkawashughulisha watu nayo.

Watu hawa wanaopekua makosa yao wao wana makosa yenye kufunika mlima. Wao hawaangalii makosa yao. Wao hutazama kosa la Imaam mtukufu ambaye Allaah Amenufaisha watu kupitia kwake na elimu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020