Makosa Kumtakia Rehema an-Nawawiy?

Swali: Kuna mwanafunzi mwanamke na mlinganizi anaona uzito kumtakia rehema Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah). Anaona kuwa huku ni kutokuwa na ghera juu ya ´Aqiydah ya Salaf na anaona kuwa hakuwa na ´Aqiydah sahihi.

Jibu: Ndugu! Hili si sahihi. Sote ni wenye kukosea na wabora katika wenye kukosea ni wale wenye kutubia. Imaam Abu Zakariyyah an-Nawawiy ni mmoja katika maimamu na katika wanachuoni wa waislamu. Alikuwa ni mwenye kuichunga dini na waislamu. Alikuwa amebobea katika elimu ya Kishari´ah. Alikuwa Faqiyh, Muhaddith, mwanachuoni wa lugha na sarafu. Alikuwa na maoni mazuri na yaliyosalimika.

Wacha tuseme kuwa alikosea katika kuzifasiri kimakosa sifa za Allaah. Lakini ni mwenye kupewa udhuru. Mazuri yake na fadhila zake zinafunika makosa yake. Ni mmoja katika maimamu. Mtakie rehema na muombe Allaah amrehemu. Waislamu wanampenda na wanamuombea du´aa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=156302
  • Imechapishwa: 19/11/2016