Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu.” Naomba nitajia majina makusudio ya “Makhaliyfah waongofu”?

Jibu: Ni wale wane; Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy. Hawa ndio Makhaliyfah waongofu.

Imesemekana kuwa ukhaliyfah wa al-Hasan bin ´Aliy ni wenye kukamilisha uongozi wa Makhaliyfah waongofu. Imesemekana vilevile kuwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) ndiye Khaliyfah wa tano. Lakini lenye kujulikana ni kwamba ni wane. Uongozi wa al-Hasan (Radhiya Allaahu ´anh) ni wenye kukamilisha na hauko kivyake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_12.mp3
  • Imechapishwa: 23/06/2018