Makatazo ya mtu kuuza asichomiliki

Swali: Ni ipi maana ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Usiuze usichomiliki?”

Jibu: Mtu akauza bidhaa ambayo hana. Kwa mfano mtu akauza gari ilihali bado hajainunua. Kitu kama hichi hufanyika kati ya watu. Utamuona mtu anauza gari, mifuko ya sukari au mchele ilihali hana nao ambapo akapokea pesa au thamani kisha ndio akaenda kununua bidhaa hiyo. Hili halijuzu. Ni lazima kwa mtu kununua bidhaa hiyo kwanza halafu ndio iandae kwa ajili ya ununuzi baada ya kuinunua. Aende zake kisha aje wakati mwingine baada ya kuinunua. Akitaka kuiuza ni vizuri. Vinginevyo awauzie wengine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (08) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191309#219638
  • Imechapishwa: 19/01/2019