Usiongee bila ya elimu, usiitafute elimu bila ya milango yake, usiichukue elimu kwa watu wasiostahiki, usitosheke na kusoma vitabu; unadai kuwa umekuwa mwanachuoni. Unahifadhi tu na wala hufahamu kitu. Haitoshi kuhifadhi tu. Ni lazima ufahamu na uwe na maarifa. Hii ni njia potofu na ni njia ya watu wapotofu. Tunamuomba Allaah afya. Ni juu ya vijana wetu – Allaah awawafikishe, kulipa umuhimu suala hili na wakae kwa wanachuoni na wasikilize kutoka kwao na wachukue elimu kutoka kwa watu wake. Wasiichukue kutoka katika fahamu zao, vitabu vyao na kwa wenzao katika wale wasiojua.

لَوْ هَدَانَا اللّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ

“Lau Allaah angelituongoa, basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni.” (14:21)

Watasema hivi siku ya Qiyaamah.

لَوْ هَدَانَا اللّهُ لَهَدَيْنَاكُمْ

“Lau Allaah angelituongoa, basi hapana shaka nasi tungelikuongoeni.”

Enyi ndugu zangu! Mtanabahi hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=RCYlyCCgp1U
  • Imechapishwa: 10/04/2022