Makatazo ya kuswali na mavazi yasiyositiri vizuri

Swali: Tuko katika wakati wa joto ambapo watu wengi wanavaa nguo nyepesi na suruwali fupi. Ni ipi hukumu ya swalah za watu hawa ikiwa kile alichokivaa kinaonyesha fomu au kinaonyesha zile sehemu ambazo hazitakiwi kuonekana?

Jibu: Miongoni mwa sharti ya kusihi kwa swalah mwanaume afunike yaliyo kati ya kitovu na magoti kwa kivazi kipana kisichoonyesha nyuma yake rangi ya ngozi. Alichoashiria muulizaji ni kweli kipo. Wako ambao wanava mavazi mepesi na hakuna alichovaa isipokuwa suruwali nyepesi na fupi isiyofunika isipokuwa tu ile sehemu ya juu ya mapaja na sehemu iliyobaki yote ya chini inakuwa wazi na watu wanaweza kuiona kiasi cha kwamba wakajua ile ngozi ilioko chini yake ni nyekundu, nyeusi au chokoleti. Hiki hakisitiri na wala haisihi kuswali nacho. Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu awe makini katika masuala haya na anawanasihi nduguze ambao wanazembea kwa sababu masuala haya si mepesi. Mimi hivi sasa nataka kuwauliza: mtu akivaa kikoi kipana na akaswali na huku juu amevaa flana, je, swalah yake inasihi au hapana? Inasihi. Bali hata kama hatokuwa na flana swalah yake inasihi. Kwa sababu kilichomuhimu ni yeye afunike yaliyo kati ya kitovu na magoti.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1230
  • Imechapishwa: 15/09/2019