Makatazo ya kula ribaa na kutotekeleza nadhiri katika Biblia

19Usimkopeshe ndugu yako Mwisraeli kitu kwa riba; usimtoze riba juu ya mkopo wa fedha, chakula, au chochote ambacho watu hukopesha kwa riba. 20Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.

21Unapoweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, usichelewe kuitekeleza, maana Mwenyezi Mungu, Mungu wako ataidai kwako, nawe utakuwa na kosa. 22Lakini ukiacha kuweka nadhiri hutakuwa na dhambi. 23Uwe mwangalifu kutimiza nadhiri uliyotamka kwa mdomo wako, maana ulimwahidi Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa hiari yako.

  • Marejeo: Kumbukumbu la Sheria 23:19
  • Imechapishwa: 03/02/2020