Swali: Nimesikia katika Hadiyth kwamba haijuzu kukunja nywele na nguo ndani ya swalah. Je, haya ni kweli?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kutozifunga nywele wala nguo. Amesema:

“Nimeamrishwa kusujudia juu ya viungo saba na tusikunje nywele wala nguo.”

Kwa hiyo muumini wakati anaposwali anatakiwa asikunje chochote. Anaposujudu basi aziache nywele na nguo zake zisujudu pamoja naye kama yuko na nywele ndefu au nguo yenye mikono mirefu. Asikunje mikono ya nguo, asikunje nywele wala asikunje kanzu yake. Hayo yanamuhusu pia mwanamke. Asikunje nguo yake. Kuhusu nywele zake ni lazima azifunike kwa sababu hazitakiwi kuonekana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4339/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%83%D9%81-%D8%A7%D9%84%D8%AB%D9%8A%D8%A7%D8%A8-%D8%A7%D9%88-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D8%B9%D8%B1-%D8%A7%D8%AB%D9%86%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 02/06/2020