Makatazo ya kukidhi haja kwa kuelekea Qiblah

Swali: Ni ipi hukumu ya kukielekea Qiblah na kukipa mgongo ndani ya nyumba na jangwani wakati wa kukidhi haja? Baadhi ya nyumba zimetengenezwa vyoo vikielekea Qiblah.

Jibu: Haijuzu kukielekea Qiblah na kukipa mgongo wakati wa kukidhi haja ni mamoja mtu anakidhi haja ndogo au kubwa akiwa mtu yuko jangwani. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikataza hilo kupitia kwa Abu Ayyuub al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) na wengineo.

Mtu ndani ya majumba hakuna neno kufanya hivo. Hilo ni kutokana na yale yaliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba amesema:

“Nilimwona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa nyumbani kwa Hafswah akikidhi haja yake hali ya kuelekea Shaam na hali ya kuipa mgongo Ka´bah.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/35)
  • Imechapishwa: 03/08/2021