Swali: Wako ambao wanatoa makarona katika Zakaat-ul-Fitwr badala ya kutoa mchele, kwa sababu imekuwa ndio chakula cha kawaida katika baadhi ya miji. Je, inajuzu kufanya hivo?

Jibu: Nchi ambayo chakula chao cha kawaida ni makarona, watatoa chakula hicho cha kawaida. Kuhusu nchi ambayo haina makarona, haisihi kutoa chakula hicho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (17) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdtf-08011435.mp3
  • Imechapishwa: 13/10/2019